Ndondo Cup 2025 Zawadi Zafikia Milioni 30 kwa Bingwa

Ndondo Cup 2025 Zawadi Zafikia Milioni 30 kwa Bingwa: Droo Rasmi ya Ndondo Cup 2025 | Shaffih Dauda Akitangaza Zawadi Kubwa Kwa Mshindi

Mashindano maarufu ya soka ya vijana Tanzania, Ndondo Cup 2025, yameingia rasmi hatua ya makundi kufuatia droo hiyo. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanamichezo mbalimbali, mwanzilishi wa mashindano hayo Shaffih Dauda alitangaza kuongeza fedha za zawadi kwa timu zilizofanya vizuri msimu wa 2025.

Ndondo Cup 2025 Zawadi Zafikia Milioni 30 kwa Bingwa

Akizungumza mara baada ya droo, Shaffih Dauda alisema:

“Msimu wa kwanza tulianza kwa kumpa bingwa Tsh milioni 3, na mwaka jana tukafika hadi Tsh milioni 25, lakini kwa mwaka huu Bingwa atapata Tsh Milioni 30 na Milioni 15 kwa mshindi wa pili.”

Zaidi ya zawadi kwa mshindi na mshindi wa pili, Dauda pia alieleza kuwa mashindano haya sasa yanazidi kuwa na mvuto na hamasa kwa timu nyingi kutokana na mfumo mpya wa utoaji zawadi kwa timu zote zinazofikia hatua ya 32 bora.

Ndondo Cup 2025 Zawadi Zafikia Milioni 30 kwa Bingwa
Ndondo Cup 2025 Zawadi Zafikia Milioni 30 kwa Bingwa

Mgawanyo wa Zawadi Ndondo Cup 2025:

  • 🏆 Bingwa: Tsh Milioni 30

  • 🥈 Mshindi wa Pili: Tsh Milioni 15

  • 🎖 Timu 32 Bora (zikitoka hatua ya makundi): Tsh Laki 5 kila moja

  • 🏅 Timu 16 Bora: Tsh Milioni 1 kila moja

  • Timu za Robo Fainali: Tsh Milioni 1.5 kila moja

  • 🥉 Timu za Nusu Fainali: Tsh Milioni 2 kila moja

Mashindano ya Ndondo Cup yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa vipaji chipukizi kuonekana, huku yakiimarika mwaka hadi mwaka kwa ubora wa maandalizi na thamani ya zawadi.

CHECK ALSO:

  1. Tetesi za Simba Kumsajili Lassine Kouma Kuziba Nafasi ya Viungo Walioondoka
  2. Che Malone Fondoh Aondoka Simba, Ajiunga na USM Alger
  3. Mohamed Hussein Kuondoka Simba Baada ya Miaka 11, Aelekea Yanga
  4. Usajili Mpya wa Simba SC 2025/2026