Ngao ya Jamii 2025, Waamuzi wa Mechi ya Yanga dhidi ya Simba

Ngao ya Jamii 2025, Waamuzi wa Mechi ya Yanga dhidi ya Simba: SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Clifford Ndimbo, limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Ngao ya Jamii 2025, Waamuzi wa Mechi ya Yanga dhidi ya Simba

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ahmed Arajiga ndiye atakuwa mwamuzi wa mechi hiyo. Atasaidiwa na Mohamed Mkono na Kasimu Mpanga. Mwamuzi wa akiba atakuwa Ramadhan Kayoko, wakati Soud Abdi atakuwa mwamuzi.

Mchezo huu unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka nchini kutokana na mchuano mkali wa kihistoria kati ya klabu hizo mbili kubwa za Tanzania. Umati mkubwa unatarajiwa kuhudhuria mechi hii, ambayo pia inaashiria kuanza kwa msimu mpya wa soka.

Ngao ya Jamii 2025, Waamuzi wa Mechi ya Yanga dhidi ya Simba

Waamuzi wa mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii 2025 kati ya Simba dhidi ya Yanga:

✅ Mwamuzi: Ahmed Arajiga
✅ Msaidizi 1: Mohamed Mkono
✅ Msaidizi 2: Kassim Mpanga
✅ Mwamuzi wa akiba: Ramadhan Kayoko

CHECK ALSO:

  1. Kagame Cup 2025 Wachezaji Waliopewa Tuzo
  2. Ratiba ya Vilabu vya Tanzania katika Mashindano ya Kimataifa
  3. Ngao ya Jamii Tanzania, Simba na Yanga
  4. Ngao ya Jamii 2025, Simba SC vs Yanga SC Historia na Rekodi