Orodha Ya Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025 | Serikali Yatangaza Walimu Wapya 189, Orodha na Maagizo Muhimu.
Serikali ya Tanzania kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imetangaza kuwataka walimu wapya 189 waliofanyiwa usaili kati ya Januari 5, 2025 na Februari 24, 2025. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya walimu waliokuwa kwenye orodha ya wasubiri na sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Tangazo hili lilitolewa rasmi Ijumaa, Machi 21, 2025 na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, likionyesha kwamba waombaji waliofaulu wanapaswa kuchukua barua zao za kazi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kutangazwa.
Orodha Ya Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025
Maeneo ya Walimu Kupangiwa Kazi
Katika awamu hii, walimu waliopangiwa kazi watahudumu katika halmashauri tano zifuatazo:
Manispaa ya Shinyanga
Wilaya ya Rorya
Manispaa ya Kahama
Wilaya ya Nyang’hwale
Wilaya ya Bukombe
HAYA HAPA MAJINA
Maelekezo kwa Walimu Walioitwa Kazini

Mahali pa Kuchukua Barua za Kazi:
Walimu wanapaswa kuchukua barua zao katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwenye Majengo ya Dk. Asha Rose Migiro, Masjala ya Wazi.
Muda wa kuchukua barua hizo ni ndani ya siku saba kuanzia Machi 21, 2025.
Njia Mbadala ya Kupata Barua:
Kwa wale ambao hawataweza kuchukua barua zao kwa wakati, barua hizo zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Tangazo hili limekuja ikiwa ni siku tisa tu baada ya Serikali kuwataka walimu wengine 319 wa fani mbalimbali, na halmashauri saba kupokea ajira mpya/Orodha Ya Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025.
Walimu wote walioajiriwa wanashauriwa kukusanya barua zao kwa wakati na kuhakikisha wanaripoti kazini kwa kufuata taratibu zilizowekwa. Serikali inaendelea kushughulikia suala la ajira katika kada mbalimbali ili kuhakikisha upungufu wa watumishi katika sekta ya elimu unafikiwa ipasavyo.
Weka maoni yako