Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF

Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF:  Serikali yaipa Simba SC Ndege Maalum ya Kusafiri kwenda Morocco kwa ajili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2025.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Rais wake Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, imetangaza rasmi kutoa ndege maalum kwa Klabu ya Simba SC kwa ajili ya kwenda Morocco kushiriki mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 17, 2025.

Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 8, 2025 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, alipokuwa akizungumza Bungeni mjini Dodoma. Uamuzi huu wa serikali unalenga kupunguza changamoto za uchovu na safari ndefu ambazo wachezaji wa Simba wangekumbana nazo iwapo wangetumia ratiba ya safari za ndege za abiria katika nchi kadhaa.

Profesa Kabudi alieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kusaidia mafanikio ya Simba SC na kuwawekea mazingira rafiki ya kiushindani katika ngazi ya kimataifa. Alisema:

Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF
Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF

Kufuatia mafanikio makubwa ya Simba na sasa kukabiliwa na mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba inasafiri hadi Morocco kumenyana na RS Berkane. Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dk.Samia imeamua kutoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha Klabu ya Simba hadi Morocco kwa ajili ya mechi hiyo/Rais Samia Aipatia Simba Ndege Maalum Kwenda Morocco kwa Mchezo wa Fainali CAF.

Simba SC imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika CAF tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo jambo ambalo limeipandisha hadhi nchi hiyo kwenye ramani ya soka barani Afrika. Serikali imetambua mafanikio hayo kuwa ni fahari ya taifa na mfano bora wa kuigwa katika sekta ya michezo.

CHECK ALSO: