Ratiba Rasmi ya Fainali za CAF 2024/2025 | Ratiba Rasmi ya Fainali za Michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/2025.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi ratiba ya mechi za mwisho za mashindano ya vilabu 2024/2025. Mechi hizi zinatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu, huku timu bora barani Afrika zikitarajiwa kuonyesha ubora wao.
Ratiba Rasmi ya Fainali za CAF 2024/2025
Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League)
Katika fainali ya Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itamenyana na Pyramids FC ya Misri katika mechi mbili:
Mchezo wa Kwanza:
Mei 24, 2025 | Sundowns vs PyramidsMchezo wa Marudiano:
Juni 1, 2025 | Pyramids vs Sundowns
Mashabiki wa soka kote barani Afrika wana matarajio makubwa huku wakisubiri kuona ni nani atatwaa taji hilo lenye heshima kubwa katika soka la vilabu barani Afrika.

Kombe la Shirikisho Afrika
Katika fainali ya Kombe la Shirikisho, Simba SC ya Tanzania itamenyana na RS Berkane ya Morocco:
Mchezo wa Kwanza:
Mei 17, 2025 | RS Berkane vs Simba SCMchezo wa Marudiano:
Mei 25, 2025 | Simba SC vs RS Berkane
Kwa Simba SC, hii ni fursa ya kihistoria ya kuandika upya rekodi yao kwenye mashindano ya CAF kwa kujaribu kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF 2024/2025 inaahidi kuwa tamasha la hali ya juu, huku timu bora zaidi za Afrika zikipambana kuwania kilele cha mafanikio ya soka barani humo. Mashabiki wote wanatarajiwa kushuhudia historia mpya ikiandikwa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako