Ratiba ya CECAFA Beach Soccer 2025, Tanzania Kuanza Dhidi ya Seychelles

Ratiba ya CECAFA Beach Soccer 2025, Tanzania Kuanza Dhidi ya Seychelles: Ratiba ya Mechi Kuanza Julai 16 mjini Mombasa

Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza ratiba rasmi ya uzinduzi wa michuano ya CECAFA Beach Soccer Championship 2025, itakayofanyika Mombasa nchini Kenya kuanzia Julai 16-20, 2025.

Ratiba ya CECAFA Beach Soccer 2025, Tanzania Kuanza Dhidi ya Seychelles

Jumla ya nchi saba zitashiriki, zikiwa zimegawanywa katika makundi mawili:

  • Kundi A: Kenya, Malawi, Burundi, Zanzibar

  • Kundi B: Tanzania, Uganda, Seychelles

Ratiba ya Mechi za Makundi

Ratiba ya CECAFA Beach Soccer 2025, Tanzania Kuanza Dhidi ya Seychelles
Ratiba ya CECAFA Beach Soccer 2025, Tanzania Kuanza Dhidi ya Seychelles

Match Day 1 – Julai 16, 2025

  • Tanzania vs Seychelles – Saa 7:30 mchana

  • Malawi vs Burundi – Saa 9:00 alasiri

  • Kenya vs Zanzibar – Saa 10:30 alasiri

Match Day 2 – Julai 17, 2025

  • Zanzibar vs Malawi – Saa 7:30 mchana

  • Burundi vs Kenya – Saa 9:00 alasiri

  • Uganda vs Tanzania – Saa 10:30 alasiri

Match Day 3 – Julai 18, 2025

  • Seychelles vs Uganda – Saa 7:30 mchana

  • Zanzibar vs Burundi – Saa 9:00 alasiri

  • Kenya vs Malawi – Saa 10:30 alasiri

Hatua ya Nusu Fainali – Julai 19, 2025

  • Semi Fainali 1: Mshindi Kundi B vs Nafasi ya Pili Kundi A – Saa 9:00 alasiri

  • Semi Fainali 2: Mshindi Kundi A vs Nafasi ya Pili Kundi B – Saa 10:30 alasiri

Fainali – Julai 20, 2025

  • Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu – Saa 9:00 alasiri

  • Fainali kuu – Saa 10:30 alasiri

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni itaanza kampeni yake dhidi ya Shelisheli Julai 16, kabla ya kumenyana na Uganda katika mchezo wa pili wa Kundi B. Kundi A, wenyeji Kenya, watamenyana na Zanzibar siku hiyo hiyo.

Michuano hii ya kihistoria inalenga kuendeleza soka la ufukweni katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kuwapa wachezaji wenye vipaji fursa ya kutambulika kimataifa.

CHECK ALSO:

  1. Himid Mao Mkami Karibu Kujiunga Tena na Azam
  2. Diogo Jota Afariki Dunia kwa Ajali ya Barabarani Akiwa na Umri wa Miaka 28
  3. Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily SC ya Misri
  4. Tanzania Prisons Yajihakikishia Kubaki Ligi Kuu NBC 2025/2026