Ratiba ya CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 | Ratiba ya Raundi ya Nne ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara La CRDB. Timu ya Singida Black Stars inatinga fainali ya Kombe la FA 2025 na inatarajiwa kuvaana na Yanga SC
Timu ya Singida Black Stars (Singida BS) imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA 2025 (CRDB Federation Cup) baada ya kuifunga Simba SC mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara.
Singida BS walionyesha kiwango cha hali ya juu na umakini mkubwa katika mchezo wa nusu fainali, hivyo kuwawezesha kuiondoa Simba SC, moja ya timu kubwa yenye historia ndefu ya mafanikio katika soka la Tanzania.
Ratiba ya CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
RATIBA YA FAINALI: Singida Black Stars vs Yanga SC
Kwa mafanikio hayo, Singida Black Stars itamenyana na Yanga SC katika fainali hii ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Yanga SC ilifuzu mapema baada ya kushinda nusu fainali ya kwanza, hivyo kujiandaa na fainali sawa na mpinzani wao mpya.
29/06/2025: 20:15 – Yanga SC VS Singida Big Stars | Amani Stadium, Zanzibar

Ratiba hii inajumuisha mechi kali zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkali, hususan michezo ya timu kubwa kama Simba SC na Yanga SC, ambayo itaamua hatma yao katika michuano ya msimu huu. Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kuona matokeo ya raundi hii ya nne.
CHECK ALSO:
					
							
							







Weka maoni yako