Ratiba ya Fainali ya Samia Womens Super Cup 2025 | Yanga Princess vs JKT Queens: Fainali ya Samia Women’s Super Cup 2025 inaelekea ukingoni
Michuano ya Samia Women’s Super Cup 2025 inakaribia kumalizika baada ya mchujo mkali wa nusu fainali uliochezwa Machi 4, 2025 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, Arusha. Timu za Yanga Princess na JKT Queens zimefanikiwa kufuzu hatua ya fainali na sasa zitachuana kuwania ubingwa wa mashindano hayo yenye heshima kubwa.
Ratiba ya Fainali ya Samia Womens Super Cup 2025
Matokeo ya nusu fainali
Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Yanga Princess walionyesha ubabe mkubwa kwa kuizaba Fountain Gate Princess mabao 7-0, ushindi mkubwa ulioifanya kuwa miongoni mwa timu zenye safu kali ya ushambuliaji kwenye mashindano haya.
Kwa upande mwingine, JKT Queens ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Simba Queens katika mchezo mgumu na uliokuwa na ushindani mkubwa. Ushindi huo umeihakikishia JKT kutinga fainali na kupata nafasi ya kutwaa taji la Samia Women Super Cup 2025.

Fainali inayofuata: Yanga Princess vs JKT Queens
Baada ya mechi hizi za nusu fainali, fainali rasmi sasa itakuwa kati ya Yanga Princess na JKT Queens. Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua sana kutokana na rekodi za timu zote mbili.
- Yanga Princess inaingia fainali ikiwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao mengi, huku ikionyesha safu kali ya ushambuliaji.
- JKT Queens kwa upande wao wanafahamika kwa uimara wa safu yao ya ulinzi na uwezo wa kushinda mechi ngumu, kama ilivyoonekana dhidi ya Simba Queens.
Mashabiki wa soka la wanawake wanatarajia pambano kali na la kusisimua huku bingwa mpya wa Samia Women’s Super Cup 2025 akitarajiwa kupatikana. Ni fainali ambayo haitakiwi kukoswa! Ratiba ya Fainali ya Samia Womens Super Cup 2025
CHECK ALSO:
Weka maoni yako