Ratiba ya Fainali za Ligi Kuu ya Vijana U20 NBC 2025

Ratiba ya Fainali za Ligi Kuu ya Vijana U20 NBC 2025: Timu 8 Kufuzu Fainali za U20 NBC Youth League 2025.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza fainali za Ligi ya Vijana ya NBC U-20 2025 zitafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 19 hadi 29, 2025, kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Clifford Mario Ndimbo, Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, timu nane (8) zimethibitishwa kufuzu hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Ratiba ya Fainali za Ligi Kuu ya Vijana U20 NBC 2025

Ratiba ya Fainali za Ligi Kuu ya Vijana U20 NBC 2025
Ratiba ya Fainali za Ligi Kuu ya Vijana U20 NBC 2025

Timu Zilizofuzu Fainali ni:

  1. Azam FC
  2. Dodoma Jiji
  3. Kagera Sugar
  4. Young Africans
  5. Kengold FC
  6. Simba SC
  7. Fountain Gate
  8. Tanzania Prisons

TFF imetangaza kuwa droo ya hatua ya makundi na ratiba rasmi ya michuano hiyo itafanyika Jumatano Mei 14, 2025.

Kila kundi litakuwa na timu kadhaa, huku timu mbili za juu kutoka kila kundi zikifuzu kwa nusu fainali kabla ya kutinga fainali kuu ya shindano hilo.

Mashindano haya ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya soka la vijana nchini, lengo likiwa ni kukuza vipaji na kuandaa wachezaji kwa ajili ya soka la kulipwa katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

CHECK ALSO: