Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar 2025/2026: SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF) limetoa rasmi ratiba ya ligi ya msimu wa 2025/2026 inayojumuisha tarehe muhimu za mechi na mashindano mbalimbali ya Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Kwa mujibu wa ratiba, maandalizi yalianza Agosti 2025 kwa usajili wa wachezaji, mafunzo ya waamuzi, na warsha kwa viongozi na makocha. Hii ni sehemu ya lengo la kuhakikisha ligi inaanza vyema na kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar 2025/2026
Matukio Muhimu Yaliyoainishwa Katika Kalenda ya ZFF 2025/2026:

-
Septemba 13, 2025 – Mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Zanzibar (PBZ Premier League).
-
Septemba 20, 2025 – Wiki ya kwanza ya ligi zote kuu na za daraja la kwanza.
-
Novemba 2025 – Ratiba inaingiliana na dirisha la FIFA la mechi za kimataifa na droo ya michuano ya FA Cup.
-
Desemba 2025 – Michuano ya Mapinduzi Cup kufanyika kati ya Desemba 28, 2025 na Januari 15, 2026.
-
Januari 2026 – Mashindano ya AFCON 2025 yataathiri kalenda, huku pia raundi za FA Cup zikichezwa.
-
Machi 2026 – Raundi ya 16 bora ya FA Cup na robo fainali.
-
Aprili 2026 – Mechi za nusu fainali ya FA Cup na Mapinduzi Cup zikifanyika.
-
Mei 2026 – Fainali za FA Cup Zanzibar, zikitarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha msimu.
-
Juni 2026 – Ligi itafikia tamati, sambamba na ratiba ya Kombe la Dunia FIFA 2026.
Kalenda ya ZFF msimu wa 2025/2026 imepangwa kwa umakini ili kumudu mashindano ya ndani na nje ya nchi. Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanaweza kutarajia ushindani mkali, kuibua vipaji vipya na burudani ya hali ya juu katika msimu mzima/Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar 2025/2026.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako