Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League

Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League | Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) inatarajiwa kurejea rasmi Ijumaa Mei 2, 2025, huku Simba SC ikikabiliwa na mfululizo wa mechi muhimu dhidi ya timu kadhaa.

Ratiba iliyotolewa kupitia Bodi ya Ligi Tanzania TPBL inaonyesha kuwa Simba SC itakuwa na jumla ya mechi nne kwa muda wa siku kumi na moja, ikitabiri ushindani mkubwa na kuhitaji maandalizi ya hali ya juu kwa wachezaji na wafanyakazi wa kiufundi.

Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League

  • Mei 02, 2025: Simba SC vs Mashujaa FC
    – Mechi hii itafungua pazia la kurejea kwa NBC Premier League baada ya mapumziko. Simba SC itakuwa mwenyeji wa Mashujaa FC, timu inayopambana kusalia ligi kuu.

  • Mei 05, 2025: JKT Tanzania vs Simba SC
    – Simba SC itasafiri kumenyana na JKT Tanzania katika uwanja wa Meja Isamuyo, ambapo ushindani mkali unatarajiwa kutokana na historia ya timu hizo katika uwanja wa nyumbani wa JKT.

Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League
Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League
  • Mei 08, 2025: Simba SC vs Pamba Jiji FC
    – Hii ni mechi nyingine ya nyumbani kwa Simba dhidi ya Pamba Jiji kutoka Mwanza. Mchezo huu unaweza kuwa muhimu kwa kuamua nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kwa Simba.

  • Mei 11, 2025: KMC FC vs Simba SC
    – Mechi ya mwisho kwa mwezi Mei kwa upande wa Simba SC itakuwa dhidi ya KMC FC (Kino Boys), ambao wamekuwa wagumu kupambana nao hususani kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mei 2025 ni wakati muhimu kwa Simba SC, ambapo kila pointi inajikita katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC. Mashabiki na wapenda soka wafuatilie kwa karibu kila mechi huku wakitarajia ushindani wa hali ya juu kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi/Ratiba ya Mechi za Simba SC Mwezi Mei 2025 NBC Premier League.

CHECK ALSO: