Ratiba ya Mechi za Twiga Stars 2025: Mechi za Kirafiki za Kimataifa za Wanawake Mei 30 na Juni 2, 2025. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars na timu ya taifa ya wanawake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) .
Mechi hizo ni sehemu ya ratiba ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kimataifa kwa wanawake na inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Ratiba ya Mechi za Twiga Stars 2025
Tanzania (Twiga Stars) vs DR Congo
π Tarehe: Mei 30, 2025
π Muda: Saa 2:00 usiku (20:00 HRS)
π Uwanja: Azam Complex, Dar es Salaam

Tanzania (Twiga Stars) vs DR Congo
π Tarehe: Juni 2, 2025
π Muda: Saa 2:00 usiku (20:00 HRS)
π Uwanja: Azam Complex, Dar es Salaam
Mashabiki wa soka hasa wa soka la wanawake wafuatilie kwa karibu mechi hizi mbili kati ya Twiga Stars na DR Congo. Hii ni fursa muhimu kwa Tanzania kuonesha maendeleo ya soka la wanawake na kutoa mwanya kwa vipaji vya ndani kungβara kimataifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako