Ratiba ya Mechi za Yanga SC Mwezi Juni 2025

Ratiba ya Mechi za Yanga SC Mwezi Juni 2025 | Klabu ya Yanga Sports Club (Yanga SC) ambayo ni moja ya klabu kongwe nchini Tanzania imetangaza ratiba ya mechi zake za Juni 2025.

Ratiba ya Mechi za Yanga SC Mwezi Juni 2025

Ratiba hiyo inajumuisha mechi mbili muhimu za Ligi Kuu ya NBC, pamoja na fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

1. Yanga SC dhidi ya Tanzania Prisons – Juni 18, 2025 (Ugenini)

Mechi ya kwanza ya mwezi huu itachezwa Juni 18, 2025 dhidi ya Tanzania Prisons. Mechi hii itachezwa ugenini saa 10:00 Jioni (4:00 PM ET) katika uwanja wa Sokoine. Hii ni mechi muhimu kwa Yanga SC inayowania kupata pointi katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Ratiba ya Mechi za Yanga SC Mwezi Juni 2025
Ratiba ya Mechi za Yanga SC Mwezi Juni 2025

2. Yanga SC dhidi ya Dodoma FC – Juni 22, 2025 (Nyumbani)

Mechi ya pili ni dhidi ya Dodoma FC, Mechi hii itachezwa Juni 22, 2025, kwenye Uwanja wa Yanga SC, pia kuanzia saa 10:00 Jioni. Mechi hii ni fursa kwa mashabiki wa nyumbani kutazama timu yao ikipigania ushindi muhimu na kumalizia msimu huu wa 2024/2025.

3. Fainali ya ASFC – Dhidi ya Singida Black Stars (Tarehe TBC)

Yanga SC nayo itacheza fainali ya CRDB dhidi ya Singida Black Stars. Hii ni fursa nyingine kwa klabu hiyo kuongeza kombe jingine katika ukusanyaji wake wa makombe. Tarehe na kiwanja rasmi cha fainali hiyo bado haijatangazwa, hivyo mashabiki wanashauriwa kukaa mkao wa kula kwa taarifa zaidi kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

CHECK ALSO: