Ratiba ya Raundi ya Awali Mashindano CAF 2025/26 | SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza tarehe rasmi za kuanza kwa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la CAF kwa msimu wa 2025/26.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CAF, duru hiyo itaanza Septemba 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kampeni mpya za mashindano ya vilabu barani Afrika.
Ratiba ya Raundi ya Awali Mashindano CAF 2025/26
Ratiba ya Mechi za Raundi ya Awali
Mchezo wa Kwanza (First Leg): Kuanzia Septemba 19 hadi 21, 2025
Mchezo wa Marudiano (Second Leg): Kuanzia Septemba 26 hadi 28, 2025
Ratiba hii imepangwa kwa kuzingatia mabadiliko yaliyofanywa na CAF ili kuendana na mashindano ya CHAN (African Nations Championship) yanayotarajiwa kuchezwa pia katika kipindi hicho.

CAF imerekebisha tarehe za mashindano haya ili kuepusha upangaji wa migogoro kati ya vilabu na timu za taifa. CHAN, ambayo inashiriki ligi za ndani pekee, inahitaji maandalizi ya kina, na wachezaji wengi wanaoshiriki katika CAF pia huchezea timu za taifa za CHAN.
Kwa hivyo, uamuzi wa kuanza kwa awamu ya awali mnamo Septemba unalenga kutoa fursa ya kujiandaa vya kutosha kwa CHAN bila kuathiri ratiba ya mashindano ya vilabu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako