Real Betis Waichapa Madrid kwa Mara ya Kwanza Baada ya Miaka 5

Real Betis Waichapa Madrid kwa Mara ya Kwanza Baada ya Miaka 5 | Real Madrid Yadondosha Pointi kwa Real Betis, Barcelona Yaendelea Kuongoza La Liga, Isco Aipa Real Betis Ushindi Dhidi ya Klabu Yake ya Zamani, Real Madrid.

Real Betis Waichapa Madrid kwa Mara ya Kwanza Baada ya Miaka 5

Real Betis wamepata ushindi wa kihistoria dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid kwa mara ya kwanza ndani ya takriban miaka mitano. Betis waliibuka washindi 2-1 kwenye Uwanja wa Estadio Benito Villamarín mjini Seville.

Matokeo ya mechi

✅ Real Betis 2-1 Real Madrid
⚽ 10′ Brahim Díaz (Real Madrid)
⚽ 34′ Cardoso (Real Betis)
⚽ 54′ Isco (P) (Real Betis)

Real Betis Waichapa Madrid kwa Mara ya Kwanza Baada ya Miaka 5
Real Betis Waichapa Madrid kwa Mara ya Kwanza Baada ya Miaka 5

Licha ya kuanza vyema kwa bao la mapema la Brahim Díaz, Real Madrid walishindwa kudhibiti uongozi wao na kwenda kupoteza mechi. Bao la Cardoso dakika ya 34 liliwarudisha Betis kwenye mechi, kabla ya Isco kufunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 54, na kuwahakikishia wenyeji ushindi huo muhimu.

Athari kwenye msimamo wa La Liga

Kwa matokeo haya, Real Madrid wamesalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 54 sawa na vinara Barcelona baada ya kucheza michezo 25. Ushindi huu ni nyongeza kubwa kwa Real Betis katika kampeni zao msimu huu, huku pia wakionyesha ubora wao dhidi ya mojawapo ya timu bora zaidi barani Ulaya.

CHECK ALSO: