RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya Simba

RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya Simba: RS Berkane ya Morocco imeshinda Kombe la Shirikisho la CAF 2025 baada ya ushindi wa jumla wa 3-1 dhidi ya Simba SC ya Tanzania. Mchezo huo wa awamu ya pili wa fainali ulichezwa katika uwanja wa kisasa wa Zanzibar New Amaan Complex mbele ya maelfu ya mashabiki na viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk Hussein Mwinyi.

Katika mkondo wa pili, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, huku RS Berkane ikinufaika na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza. Hii ilikuwa mara ya tatu kwa RS Berkane kushinda taji la CAF, na kuwaweka miongoni mwa vilabu vilivyofanikiwa zaidi barani Afrika katika mashindano hayo.

RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya Simba

Simba SC walianza kwa kishindo mechi ya mkondo wa pili kwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo Mutale dakika ya 17. Hata hivyo, matumaini ya Wekundu hao yalififia baada ya mchezaji wao Kagoma kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 50. RS Berkane alichukua faida ya hasara ya mtu kusawazisha kupitia Sidibe katika muda ulioongezwa (90+3′).

RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya Simba
RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya Simba
  • Muda wa Mchezo: FT: Simba SC 🇹🇿 1-1 🇲🇦 RS Berkane

  • Magoli:

    • 17’ – Mutale (Simba SC)

    • 90+3’ – Sidibe (RS Berkane)

  • Kadi Nyekundu:

    • 50’ – Kagoma (Simba SC)

  • Matokeo ya Jumla: RS Berkane 3-1 Simba SC

Hii si mara ya kwanza kwa Simba SC kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Rais wa Zanzibar. Mwaka 1993 timu hiyo ilishindwa tena katika fainali ya kimataifa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni baba wa Rais wa sasa wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi. Tukio hilo linaacha kumbukumbu ya kihistoria ambayo imerudiwa baada ya miaka 32.

Kwa ushindi huu, RS Berkane itawakilisha Afrika katika Kombe la CAF Super Cup dhidi ya washindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa Simba SC, ni wakati wa kufanya tathmini na maandalizi mapya ili kujiboresha kwa ajili ya mashindano yajayo.

CHECK ALSO: