Senegal Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuifunga Sudan 3-1

Senegal Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuifunga Sudan 3-1 | Timu ya taifa ya Senegal, maarufu kama Simba wa Teranga, imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan. Mchezo huo wa hatua ya 16 bora ulipigwa katika Uwanja wa Grand de Tanger.

Senegal Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuifunga Sudan 3-1

Senegal ilianza mchezo kwa umakini mkubwa licha ya Sudan kupata bao la mapema. Dakika ya 6 ya mchezo, Abdallah aliitanguliza Sudan kwa bao la haraka, hali iliyowapa presha mabingwa hao wa Afrika. Hata hivyo, Senegal ilirejea kwa nguvu na kudhibiti mchezo kwa kiwango kikubwa.

Kiungo Idrissa Gueye aliibeba Senegal kwa kufunga mabao mawili muhimu. Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 29, kabla ya kuongeza bao la pili katika dakika ya 45+3 mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Mabao hayo yaliirudisha Senegal mchezoni na kuwapa uongozi kabla ya mapumziko.

Senegal Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuifunga Sudan 3-1
Senegal Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuifunga Sudan 3-1

Kipindi cha pili, Senegal iliendelea kucheza kwa nidhamu na umiliki mzuri wa mpira. Dakika ya 77, Mbaye alifunga bao la tatu lililohitimisha ushindi wa 3-1 na kuhakikisha tiketi ya robo fainali kwa Simba wa Teranga.

Kwa matokeo hayo, Senegal sasa itasubiri mshindi kati ya Mali au Tunisia, ambao wanatarajiwa kukutana katika mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora. Ushindi huu unaonyesha uimara na uzoefu wa Senegal katika michuano ya AFCON, huku ikipewa nafasi kubwa ya kuendelea kupigania taji hilo.

CHECK ALSO:

  1. Dirisha Dogo la Usajili Msimu wa 2025/2026 Lafunguliwa Rasmi
  2. CAF Yatangaza Kikosi Bora cha AFCON 2025 Hatua ya Makundi
  3. Makocha Wanaolipwa Mshahara Mkubwa Afrika 2026
  4. Chelsea Yaachana Rasmi na Kocha Enzo Maresca