Simba Day 2025: Simba SC Vs Gor Mahia Leo, Septemba 10, 2025, ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa Simba SC, huku klabu hiyo ikisherehekea siku ya Simba Day kwa kukitambulisha rasmi kikosi na makocha kwa msimu wa 2025/2026. Hafla hiyo inafanyika katika viwanja vya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki wenye shauku ya kuwaona wachezaji wapya na maandalizi ya msimu mpya.
Simba Day 2025: Simba SC Vs Gor Mahia Leo
Katika sherehe hizo viongozi wa klabu, wakufunzi na wachezaji wote wa Simba SC walijitambulisha kwa heshima kwa mashabiki. Huu ni utamaduni wa klabu hiyo ambayo imekuwa kivutio kikubwa cha michezo nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Shughuli ya Simba Day inafikia tamati kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambapo Simba SC itamenyana na Gor Mahia FC ya Kenya. Mechi hii ni kipimo muhimu kwa kikosi kipya cha Simba, huku ikitarajiwa kuonyesha uimara wa wachezaji wapya na mikakati ya timu ya makocha kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na michuano ya Kimataifa ya CAF.
Kwa mashabiki, Simba Day si tukio la kawaida tu, bali ni sherehe kubwa inayowapa fursa ya kushuhudia mwelekeo wa timu yao katika msimu mpya. Ni siku ya hamasa, mshikamano, na matumaini mapya kwa mashabiki wa Simba SC.
SOMA PIA:
- Taifa Stars Vs Niger Leo Saa Ngapi?
- Kikosi cha Taifa Stars Leo Vs Niger 09/09/2025
- Matokeo ya Taifa Stars Leo Vs Niger 09/09/2025
- Mishahara ya Wachezaji wa Yanga 2025/2026
Weka maoni yako