Simba Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Dhidi ya RS Berkane: Jumamosi Saa 4:00 Usiku. Simba SC imewasili rasmi Morocco tayari kwa mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji RS Berkane. Mchezo huu wa kihistoria utafanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Stade Municipal de Berkane, kuanzia saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
Mara baada ya kutua Morocco, wachezaji na makocha wa Simba SC walionyesha kujiamini huku wakitoa ujumbe mzito kwa wapinzani wao:
“Hii tunabeba.”
Simba Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Dhidi ya RS Berkane
Kauli hii inaashiria dhamira yao ya dhati ya kuweka historia ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo (Simba Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Dhidi ya RS Berkane).
Simba SC inaingia kwenye mechi hii ikijua umuhimu wa kucheza na RS Berkane ugenini. Hata hivyo, klabu hiyo ya Tanzania ina rekodi nzuri ya kushindana na timu kubwa za Afrika na imeonyesha uwezo mkubwa katika hatua za awali za michuano hii.

- Timu: RS Berkane vs Simba SC
- Tukio: Fainali ya Kwanza – CAF Confederation Cup 2024/2025
- Siku: Jumamosi
- Muda: Saa 4:00 Usiku (EAT)
- Uwanja: Stade Municipal de Berkane, Morocco
- Mbashara: Azam Sports 1 HD
Simba SC inatazamia kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika, na ushindi katika mechi hii ya ufunguzi unaweza kuwa hatua kubwa ya kutimiza ndoto hiyo.
RS Berkane ni timu yenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya CAF, ikiwa tayari imeshinda taji hili. Wakiwa nyumbani watashuka uwanjani wakiwa na nguvu za mashabiki wao kutafuta ushindi kabla ya mechi ya marudiano.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako