Simba Ilimsajili Ellie Mpanzu Kutoka AS Vita kwa Mkataba wa Miaka Miwili: Klabu ya Simba SC ya Tanzania imekamilisha usajili wa kiungo Ellie Mpanzu mwenye umri wa miaka 23 kutoka klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ada ya uhamisho ya dola za Marekani 180,000 sawa na takriban shilingi milioni 484 za Kitanzania.
Simba Ilimsajili Ellie Mpanzu Kutoka AS Vita kwa Mkataba wa Miaka Miwili
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Mpanzu alisaini mkataba wa miaka miwili unaomalizika 2026 na atakuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Usajili huu unatajwa kuwa ni mkakati wa Simba SC kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa kama vile Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kusajili mchezaji mdogo lakini mwenye uzoefu kwa klabu kubwa kama AS Vita ni hatua muhimu kuelekea kuwekeza katika vipaji vya muda mrefu na thamani ya kimkakati.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa mchezaji huyo yuko kwa mkopo Simba na amekamilisha dili la kusajiliwa moja kwa moja na klabu moja ya nchini humo.
Tumebaini hilo si kweli, na Mpanzu ni mali ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili. Kwa hiyo Simba ikiamua kumuuza au kusitisha mkataba ataweza kusajili sehemu nyingi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako