Simba Kuzindua Jezi Mpya 2025/26 Leo Saa 1:00 Usiku | Klabu ya Simba Sports Club (SSC) maarufu kwa jina la wekundu wa Msimbazi leo inatarajiwa kuzindua rasmi jezi yake mpya itakayotumika msimu wa 2025/2026. Hii ni mara ya kwanza kwa Simba SC kuzindua jezi yake mpya kwa ushirikiano na kampuni ya kimataifa ya vifaa vya michezo ya Diadora.
Simba Kuzindua Jezi Mpya 2025/26 Leo Saa 1:00 Usiku

Uzinduzi huo utafanyika saa 1:00 Usiku, ambapo mashabiki wa klabu hiyo kubwa Tanzania na Afrika Mashariki wanatarajiwa kushuhudia tukio la kihistoria la kuonyesha muonekano mpya wa jezi zitakazotumika katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Mrembo mwenye sauti ya kumtoa nyoka shimoni, Yammi atakuwepo leo Super Dome, Masaki kukuburudisha wewe ambaye utaungana na Wanasimba wenzako kwenye tukio la uzinduzi wa jezi mpya za Simba SC 2025/26.
Tiketi ya VIP ni Tsh. 250,000 (jezi tatu), Gold ni Tsh. 200,000 (jezi mbili) na… pic.twitter.com/xteXXCbC9y
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) August 31, 2025
Kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Diadora, Simba SC inatarajia kufanya vifaa vya michezo vya wachezaji wake kuwa vya kisasa, ili kuendana na ushiriki wake katika Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), na mashindano ya kimataifa ya CAF.
Mashabiki wanahimizwa kufuatilia uzinduzi huu, kwani jezi mpya huwa sehemu ya utambulisho wa klabu katika msimu mzima na mara nyingi huambatana na kampeni maalum za masoko na kijamii.
SOMA PIA:
Weka maoni yako