Simba SC vs Al Masry April 9, 2025 Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF | Saa 10:00 Jioni, Benjamin Mkapa, Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Masry Aprili 9, 2025, katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
Simba SC, maarufu kwa jina la Mnyama, inatarajiwa kushuka dimbani Jumatano Aprili 9, 2025, katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.
Simba SC vs Al Masry April 9, 2025 Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
Mchezo huo muhimu utafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 Jioni.
Simba SC inalenga kutumia faida ya nyumbani kupindua matokeo ya mkondo wa kwanza na kuhakikisha inatinga nusu fainali ya michuano hii ya kimataifa.
Klabu hiyo ya Tanzania imekuwa na rekodi nzuri inapocheza nyumbani hasa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mashabiki wao hujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.

Al Masry wanafahamu ugumu wa mechi hiyo, hasa ikizingatiwa presha ya uwanja wa wageni na hali ya joto ya mashabiki wa Simba SC. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikitafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Mashabiki wa Simba SC wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao kwa amani na nidhamu ili kuwaongezea morali wachezaji uwanjani. Hii ni mechi muhimu inayoweza kuamua hatima ya msimu wa kimataifa wa klabu hiyo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako