Simba SC Yafanya Usajili Mkubwa, Hawa Hapa Wachezaji wa Kigeni Wapya: Simba SC imefanya mabadiliko makubwa ya usajili kabla ya msimu mpya.
Simba SC Yafanya Usajili Mkubwa, Hawa Hapa Wachezaji wa Kigeni Wapya
Klabu ya Simba Sports Club imeanza msimu mpya kwa mabadiliko makubwa ya usajili hasa ujumuishaji wa wachezaji wa kigeni. Mabadiliko haya yanalenga kuimarisha ushindani wake katika Ligi Kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa, kama vile Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji wa Kigeni Waliotemwa
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Simba SC imeachana na huduma za wachezaji watano wa kigeni waliokuwa sehemu ya kikosi msimu uliopita. Wachezaji hao ni:
- Nouma π²πΌ
- Okejepha π³π¬
- Fernandez π¦π΄
- Ngoma π¨π©
- Che Malone π¨π²
Uamuzi wa kuwaacha wachezaji hao umefungua nafasi kwa usajili wa majina mapya, huku klabu ikilenga kuongeza ubora na ufanisi katika maeneo muhimu ya uwanjani.
Wachezaji Wapya Waliosajiliwa
Simba SC imetangaza usajili wa wachezaji wapya wa kigeni wenye uzoefu na uwezo wa hali ya juu, wakiwemo:
- De Reuck πΏπ¦
- Sowah π¬π
- Bajaber π°πͺ
- KantΓ© πΈπ³
- Naby Camara π¬π³
- Neo Maema πΏπ¦ ( Bado Utambulisho)

Kwa mujibu wa kanuni za usajili, klabu inaruhusiwa kuwa na wachezaji wa kigeni watano pekee. Kwa sasa Simba SC tayari imekamilisha idadi hiyo (5/5), jambo linaloashiria kuwa mchezaji mmoja wa kigeni atalazimika kuachwa ili kutoa nafasi kwa Neo Maema kujiunga rasmi.
Hali hii imezua mjadala miongoni mwa mashabiki kuhusu mchezaji gani wa kigeni ataachwa. Hata hivyo, lengo kuu la bodi ni kuhakikisha kikosi cha mwisho kinajumuisha wachezaji bora kwa msimu ujao.
Kwa mabadiliko hayo, Simba SC inatarajiwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu, kuwania mataji makubwa ndani na nje ya Tanzania, na kurejesha heshima yake ya kuwa miongoni mwa klabu muhimu barani Afrika. Mashabiki na wadau wa soka wanasubiri kwa hamu matunda ya mikakati hii mipya ya uhamisho.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako