Simba vs Dodoma Jiji Wapangiwa Tarehe Mpya Baada ya Kuahirishwa | Mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kati ya Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao awali uliahirishwa kufuatia ajali iliyohusisha timu ya Jiji la Dodoma, sasa umepangwa kuchezwa Machi 14, 2025. Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Simba vs Dodoma Jiji Wapangiwa Tarehe Mpya Baada ya Kuahirishwa
Sababu ya kuahirisha mechi
Tarehe 10 Februari 2025 basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa Dodoma Jiji FC wakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam lilizama mtoni na kusababisha majeraha kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo. Kutokana na hali hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliahirisha mechi hiyo ili kuwapa muda wachezaji walioathirika kupata nafuu.

Maandalizi ya mechi ya marudiano
Kufuatia kutangazwa kwa ratiba mpya, vilabu vyote viwili vinajiandaa kwa mechi hiyo muhimu ya ligi. Simba SC inahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa, huku Dodoma Jiji FC ikisaka matokeo mazuri baada ya kipindi kigumu cha janga na majeruhi.
Mashabiki wa soka nchini wanatarajia mchezo huo wenye ushindani mkali, macho yote yakiwa yameelekezwa kwa Simba SC kucheza nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji FC, ambao watakuwa wamejipanga kudhihirisha uimara wao licha ya changamoto walizokutana nazo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako