Simba vs RS Berkane Leo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025

Simba vs RS Berkane Leo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025: Leo usiku, Simba SC ya Tanzania itashuka dimbani nchini Morocco kumenyana na RS Berkane katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 4:00 asubuhi. Saa za Afrika Mashariki.

Simba vs RS Berkane Leo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025

Tukio hili ni la kihistoria kwa Simba SC, ambayo inawakilisha Afrika Mashariki katika kiwango cha juu kabisa cha mashindano haya ya pili kwa ukubwa barani Afrika. Mechi ya mkondo wa pili inatarajiwa kuchezwa wiki mbili zijazo jijini Dar es Salaam.

Kucheza ugenini dhidi ya RS Berkane, moja ya klabu zenye uzoefu mkubwa katika mashindano haya ni mtihani mkubwa kwa Simba SC. Berkane tayari ameshinda taji hili mara mbili katika miaka ya hivi karibuni na ana rekodi nzuri anapocheza nyumbani.

Simba vs RS Berkane Leo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025
Simba vs RS Berkane Leo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025

Simba SC inayofahamika kwa mashabiki wake kwa jina la “Mnyama” au “Lunyasi” imeonyesha uwezo mkubwa katika hatua za awali za michuano hiyo na inatarajiwa kuonyesha ukomavu mkubwa katika mchezo huu wa fainali.

Fainali ya leo ni mtihani mkubwa kwa Simba SC, si tu kuonyesha ubora wao barani Afrika, bali pia kuitangaza Tanzania katika ramani ya kimataifa ya soka. Matokeo ya mechi ya kwanza yataongeza matarajio ya mechi ya marudiano nyumbani.

CHECK ALSO: