Simba vs Singida Big Stars Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup | Simba SC itamenyana na Singida KE katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB Mei 16 na 17.
Simba vs Singida Big Stars Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup
Michuano ya CRDB Bank Federation Cup inaendelea kushika kasi baada ya timu tatu kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali, na droo itaamua mpangilio wa mechi zijazo.
Simba SC itamenyana na Singida Black Stars (Singida BS) katika moja ya mechi za nusu fainali, zinazotarajiwa kuchezwa kati ya Mei 16 na 17, 2025.
Singida BS imejihakikishia nafasi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali. Ushindi huo uliwapa tiketi ya moja kwa moja ya kuingia nne bora.
Kwa upande mwingine, JKT Tanzania ambayo tayari imetinga hatua ya nusu fainali, bado inamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Yanga SC na Stand United, utakaopigwa Jumanne hii kwenye Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 Jioni. Timu itakayoshinda mchezo huo itamenyana na JKT Tanzania katika nusu fainali nyingine.

Ratiba ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB 2025 (hadi sasa):
- Simba SC dhidi ya Singida Black Stars – Mei 16 na 17
- JKT Tanzania dhidi ya Yanga SC/Stand United – Tarehe itatangazwa
Michuano ya CRDB Bank Federation Cup inaendelea kuvutia mashabiki wengi kutokana na ushindani wa hali ya juu. Timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali zimepata fursa ya kuwania taji hilo muhimu katika soka la Tanzania, macho yote yakiwa yameelekezwa kwenye mechi kati ya Yanga SC na Stand United, itakayoamua hatima ya nusu fainali ya pili/Simba vs Singida Big Stars Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako