Simba vs Singida Big Stars Nusu Fainali CRDB Federation Cup Mei 31: MASHABIKI wa soka nchini Tanzania wanatarajia kumenyana vikali katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB, utakaowakutanisha vigogo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC dhidi ya Singida Big Stars (BS).
Simba vs Singida Big Stars Nusu Fainali CRDB Federation Cup Mei 31
Mchezo huu utafanyika Jumamosi Mei 31, 2025, kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, uliopo Mkoani Manyara, kuanzia saa 9:30 alasiri.
Hii ni hatua muhimu kuelekea fainali ya kombe kuu la taifa, ambalo limejaa ushindani kutoka kwa vilabu kadhaa. Simba SC, maarufu kwa jina la Mnyama, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya mafanikio katika mashindano ya ndani, huku Singida KE ikiwa na njaa ya kuweka historia na kufuzu kwa fainali kwa mara ya kwanza.

Kamati ya maandalizi ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB imethibitisha kuwa maandalizi yote ya mechi hiyo muhimu yanaendelea vizuri. Usalama, mauzo ya tikiti na miundombinu ya uwanja tayari imepewa kipaumbele ili kuhakikisha mashabiki wanafurahia burudani ya hali ya juu.
Mashabiki wote wa soka wanahimizwa kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa kushuhudia mtanange huo wa kusisimua kati ya wababe hao wa soka nchini.
CHECK ALSO:
- RS Berkane Yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 Jumla ya Mabao 3-1 Dhidi ya SimbaÂ
- Fainali ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika, Simba SC vs RS Berkane Leo
- Sunderland Yapanda Daraja Kucheza Ligi Kuu England Msimu wa 2025/26 Baada ya Miaka 8
- Bayer Leverkusen Yafikia Makubaliano na Eric ten Hag Kuchukua Nafasi ya Xabi AlonsoÂ
Weka maoni yako