Simba vs Singida Black Stars Leo Saa Ngapi?, Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB | Leo Mei 31, 2025 hisia za mashabiki wa soka nchini zitaelekezwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mkoani Manyara, ambapo Simba SC itamenyana na Singida KE katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.
Simba vs Singida Black Stars Leo Saa Ngapi?, Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB
Muda wa Mechi:
Mchezo huu wa kusisimua utaanza rasmi saa 9:30 Alasiri na kuonyeshwa moja kwa moja na AzamSports3HD, hivyo kuruhusu mashabiki wengi kufuatilia mechi hiyo muhimu kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
Mechi hii ina umuhimu mkubwa, si tu kwa kufuzu hadi fainali, bali pia kwa heshima ya klabu. Mshindi atajihakikishia nafasi ya kucheza fainali dhidi ya Yanga SC (Mwananchi), ambayo tayari imefuzu mapema wiki hii.
Katika nusu fainali hii, swali kuu linabaki: Je, Simba SC au Singida BS itaifuata Yanga SC katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB 2025? Majibu yote yatapatikana leo jioni katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako