Simba Yaachana na Wachezaji 7 Msimu Huu, Wale Waliosajiliwa 2024/25

Simba Yaachana na Wachezaji 7 Msimu Huu, Wale Waliosajiliwa 2024/25: Simba SC imeanza mchakato wa kupunguza wachezaji wake waliosajiliwa kwa msimu wa 2024/25 kwa kuwaachia rasmi wachezaji saba mmoja wao akiwa kwa mkopo. Hili limezua mjadala mkubwa kuhusu utendakazi wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo ikiwa ni miezi michache tu baada ya kuwasajili kwa matumaini ya kurudisha heshima ya ubingwa.

Msimu uliopita Simba ilisajili wachezaji zaidi ya 10 wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujenga kikosi imara kitakachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho Afrika. Hata hivyo, mwenendo wa sasa unaonyesha kwamba wengi wa wachezaji hawa hawajafikia kiwango kilichotarajiwa.

Simba Yaachana na Wachezaji 7 Msimu Huu, Wale Waliosajiliwa 2024/25

Orodha ya Wachezaji Waliosajiliwa Msimu wa 2024/25:

  1. Ahoua Jean Charles ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ

  2. Steven Mukwala ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ

  3. Joshua Mutale ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฒ

  4. Abdulrazak Hamza ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

  5. Debora Fernandes ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ด โ‡’ OUT

  6. Augustine Okejepha ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฌ โ‡’ OUT

  7. Valentino Mashaka ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

  8. Omary Abdallah Omary ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ โ‡’ OUT

  9. Valentin Nouma ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ซ โ‡’ OUT

  10. Karaboue Chamou ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ

  11. Yusuph Kagoma ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

  12. Awesu Ali Awesu ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

  13. Moussa Camara ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฑ

  14. Kelvin Kijili ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ โ‡’ OUT

  15. Lionel Ateba ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฒ โ‡’ OUT

Hadi sasa, wachezaji saba kati ya hawa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao, hali inayoonyesha kuwepo kwa kasoro katika mchakato wa usajili.

Simba Yaachana na Wachezaji 7 Msimu Huu, Wale Waliosajiliwa 2024/25
Simba Yaachana na Wachezaji 7 Msimu Huu, Wale Waliosajiliwa 2024/25

Idadi kubwa ya wachezaji wanaoondoka katika kipindi kifupi ni ishara ya kutoridhishwa na matokeo ya uwekezaji uliofanyika kwenye soko la uhamisho. Pia inadhihirisha mapungufu ya mfumo wa skauti na kuajiri, hasa pale wachezaji wanaosajiliwa kwa gharama kubwa wanaposhindwa kufikia viwango vya ushindani.

Kamati ya Uhamisho inapaswa kutoa majibu kwa wanachama na mashabiki waliokuwa na matarajio makubwa, hasa pale walipoamini kuwa wachezaji hao ndio โ€œsuluhisho la kutwaa ubingwa.โ€ Kiwango cha idadi hiyo kubwa ya wachezaji wanaoondoka msimu mmoja tu baada ya kusajiliwa kinaibua maswali ya msingi kuhusu mchakato mzima wa kuwatathmini wachezaji kabla ya kusajili.

Kushindwa kwa Simba

Msimu wa 2024/25, Simba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC na nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, jambo ambalo kwa mtazamo wa kimkakati, halikufikia matarajio ya uwekezaji mkubwa uliofanywa.

Iwapo Kamati ya Usajili ilikuwa na imani kuwa wachezaji iliyowasajili wangetwaa ubingwa, hoja ya kushindwa kufikia malengo inapaswa kuzingatia ubora wa usajili. Ubora wa mchezaji huamuliwa na utafiti sahihi wa soko, tathmini ya uwezo, na matumizi bora ya rasilimali.

CHECK ALSO:

  1. Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway
  2. Waamuzi Watanzania Arajiga na Ally Hamdani Wateuliwa Kwa CHAN 2024/2025
  3. KIKOSI Cha DR Congo cha CHAN 2025
  4. KIKOSI Cha Burkina Faso cha CHAN 2025