Simba Yabadili Ratiba ya Safari Kwenda Morocco kwa Fainali vs RS Berkane

Simba Yabadili Ratiba ya Safari Kwenda Morocco kwa Fainali vs RS Berkane: Simba SC Yabadilisha Ratiba ya Usafiri kwenda Morocco kwa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika

Simba SC imefanya mabadiliko ya ghafla katika ratiba yake ya safari ya kwenda Morocco, ambapo timu hiyo sasa itaondoka saa 3:00 usiku. leo Jumanne, Mei 13, 2025, kinyume na ratiba ya awali ya saa 11:00 asubuhi kama ilivyoripotiwa awali.

Mabadiliko haya yanatajwa kuwa sehemu ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya RS Berkane, utakaochezwa Mei 17, 2025 nchini Morocco.

Simba Yabadili Ratiba ya Safari Kwenda Morocco kwa Fainali vs RS Berkane

Simba Yabadili Ratiba ya Safari Kwenda Morocco kwa Fainali vs RS Berkane
Simba Yabadili Ratiba ya Safari Kwenda Morocco kwa Fainali vs RS Berkane

Mchezo wa mkondo wa pili wa fainali umepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 25, 2025, huku mshindi wa mechi zote mbili akishinda Kombe la Shirikisho la CAF 2025.

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuwa kamili, kikiongozwa na benchi la ufundi la klabu hiyo na uongozi wa juu. Maandalizi ya mwisho kabla ya safari yamejumuisha mazoezi ya kiufundi na mpango wa kukabiliana na hali ya hewa na mazingira mapya nchini Morocco.

Wataalamu wa masuala ya michezo wanazishauri timu kufanya maandalizi ya kina kabla ya mechi kubwa kama hizi, hasa kwa safari za kimataifa zinazoathiri utimamu wa wachezaji kutokana na tofauti za ratiba, hali ya hewa na mazingira ya kucheza.

CHECK ALSO: