Simba Yaibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Coastal Union 3-0 | Simba SC imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Machi 1, 2025. Ushindi huu ni muhimu kwa Simba SC inayopigania kuwania ubingwa wa ligi hiyo.
Simba Yaibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Coastal Union 3-0
Matokeo ya Mchezo
⏰ FT: Coastal Union 0-3 Simba SC
⚽ Steven Mukwala (🅰️ Duchu)
⚽ Steven Mukwala (🅰️ Mpanzu)
⚽ Steven Mukwala

Mukwala anaendelea kung’ara
MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Steven Mukwala ameibuka kinara wa mchezo baada ya kufunga mabao yote matatu (hat-trick), na kufikisha jumla ya mabao 8 kwenye Ligi Kuu msimu huu. Pia aliongeza pasi 2 za mabao, na kupata nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, akimpita Ateba.
Simba SC inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa Kariakoo derby
Baada ya ushindi huo muhimu, Simba SC sasa inajiandaa na mechi yao kubwa dhidi ya Yanga SC Machi 8, 2025, mechi inayotarajiwa kuwa na matokeo muhimu katika mbio za ubingwa.
Simba SC inaendelea kuonyesha ubora wake na mashabiki watakuwa na matumaini kuwa timu yao itaendeleza kiwango chake kizuri katika mechi zijazo. 🦁🔥
CHECK ALSO:
Weka maoni yako