Simba Yaifunga Pamba Jiji 5-1, Ahoua Kwenye Mbio za Kiatu cha Dhahabu Ligi Kuu 2025

Simba Yaifunga Pamba Jiji 5-1, Ahoua Kwenye Mbio za Kiatu cha Dhahabu Ligi Kuu 2025: Simba SC yaichapa Pamba Jiji FC mabao 5-1 huku Ahoua akiibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025.

Klabu ya Simba SC imeendelea kuonyesha nguvu zake katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Simba Yaifunga Pamba Jiji 5-1, Ahoua Kwenye Mbio za Kiatu cha Dhahabu Ligi Kuu 2025

Katika mechi hiyo ya kusisimua, mshambuliaji mahiri wa Simba SC, Jean Charles Ahoua, alifunga ‘hat trick’ (mabao matatu), na kufikisha jumla ya mabao 15 hadi sasa msimu huu na kumfanya kuwa kileleni mwa orodha ya wafungaji bora wa ligi hiyo. Ahoua alifunga penalti dakika ya 15, kisha akaongeza bao la pili dakika ya 36 na la tatu dakika ya 47.

Simba Yaifunga Pamba Jiji 5-1, Ahoua Kwenye Mbio za Kiatu cha Dhahabu Ligi Kuu 2025
Simba Yaifunga Pamba Jiji 5-1, Ahoua Kwenye Mbio za Kiatu cha Dhahabu Ligi Kuu 2025

Lionel Christian Ateba pia aliendelea kuwa tishio langoni mwa timu pinzani, akifunga mabao mawili (katika dakika ya 79 na 84), na kufikisha jumla ya mabao 12 msimu huu. Bao pekee la Pamba Jiji FC lilifungwa na mchezaji wake, Tegisi, dakika ya 87.

Matokeo ya Mchezo:
FT: Simba SC 5-1 Pamba Jiji FC
⚽ 15’ Ahoua (P)
⚽ 36’ Ahoua
⚽ 47’ Ahoua
⚽ 79’ Ateba
⚽ 84’ Ateba
87’ Tegisi ⚽

Kwa ushindi huo Simba SC imezidi kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kwa kutumia vyema mechi za ugenini. Timu hiyo sasa inaendelea kulenga kushika nafasi ya kwanza na kuweka presha kwa wapinzani wake wakubwa katika mbio za ubingwa.

CHECK ALSO: