Simba Yaifunga Stellenbosch 1-0, Mguu Mmoja Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025

Simba Yaifunga Stellenbosch 1-0, Mguu Mmoja Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025 | Simba SC Yaibwaga Stellenbosch 1-0 Zanzibar | Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2025, Mguu Mmoja

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025 baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza ya nusu fainali ilichezwa kwenye Uwanja Mpya wa Amaan Complex mjini Zanzibar Aprili 20, 2025.

Simba Yaifunga Stellenbosch 1-0, Mguu Mmoja Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025

Matokeo ya Mchezo:

  • Simba SC 🇹🇿 1-0 🇿🇦 Stellenbosch FC

  • Mfungaji: Ahoua dakika ya 45+2

Bao hilo muhimu lilifungwa katika muda wa nyongeza kabla ya mapumziko na lilitosha kuipa Simba SC ushindi muhimu wa nyumbani.

Kwa ushindi huo Simba SC ina mguu mmoja kwenye fainali, lakini mtihani mkubwa bado unasubiri katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Aprili 27, 2025 nchini Afrika Kusini.

Simba Yaifunga Stellenbosch 1-0, Mguu Mmoja Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025
Simba Yaifunga Stellenbosch 1-0, Mguu Mmoja Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025

 

Tahadhari Mashabiki na Wadau: Licha ya ushindi huo wa nyumbani, Simba SC watalazimika kucheza kwa umakini mkubwa katika mchezo wa mkondo wa pili ili kuhakikisha hawapotezi nafasi ya kihistoria ya kufuzu kwa fainali ya michuano hiyo muhimu ya Afrika kwa mara nyingine. Stellenbosch ni timu yenye uwezo mkubwa hasa wa nyumbani, hivyo maandalizi ya kimkakati yanahitajika.

Simba SC sasa inahitaji sare au ushindi wowote ugenini ili kufuzu rasmi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025. Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba wana matumaini makubwa huku wakisubiri kwa hamu mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki ijayo.

CHECK ALSO: