Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC

Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC: Klabu ya Simba Sports Club imekamilisha usajili wa beki wa kushoto Anthony Mligo, ambaye amejiunga rasmi akitokea Namungo FC.

Usajili wa mchezaji huyo umekamilika kwa mafanikio, na taarifa zinaeleza kuwa mikataba yote imesainiwa rasmi (Signed & Sealed), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba SC, Mligo anatarajiwa kusafiri wiki hii kuelekea nchini Misri, ambako kikosi cha Simba kitaweka kambi ya maandalizi ya msimu wa 2025/26.

Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC

Usajili wa Anthony Mligo unaonekana kuwa ni hatua ya kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo, hasa ikizingatiwa Simba SC inatarajiwa kushiriki Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho Afrika CAF, na michuano mingine ya ndani na nje ya nchi.

Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC
Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC

Mligo ambaye amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Namungo FC, anafika Simba akiwa na uzoefu mkubwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara na anaweza kuchangia kuongeza ushindani kwenye beki wa kushoto.

Mashabiki wa Simba SC wanatarajiwa kushuhudia kuanza kwa zama mpya kwa Mligo katika klabu yenye historia nzuri. Uongozi wa Simba umetakiwa kuhakikisha mchezaji huyo anasajiliwa katika mfumo wa CAF TMS kwa wakati ili aweze kucheza mechi za kimataifa bila vikwazo vya kiutawala.

CHECK ALSO:

  1. Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Azam TV, Agosti 9 Saa 8 Mchana
  2. Ratiba ya CHAN 2025 Leo
  3. Msimamo wa CHAN 2024/2025 Taifa Stars
  4. Tanzania Yaanza Kwa Kishindo CHAN 2024, Taifa Stars 2-0 Burkina Faso