Simba Yaondolewa CRDB Federation Cup, Singida BS vs Yanga Fainali | Simba SC yaondolewa kwenye michuano ya CRDB Bank Federation Cup 2025 baada ya kuifunga Singida Black Stars mabao 3-1.
Simba Yaondolewa CRDB Federation Cup, Singida BS vs Yanga Fainali
Simba SC imetolewa rasmi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB 2025 baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara.
FT: Simba Sc 1️⃣ ➖ 3️⃣ Singida BS
⚽️ 16′ Jonathan Sowah
⚽️ 34′ Keyekeh
⚽️ 48′ Keyekeh
⚽️ 68′ Jean Ahoua
Katika mechi hiyo ngumu, Singida Black Stars walionyesha kiwango bora na nidhamu ya hali ya juu, na kuwawezesha kupata ushindi mnono dhidi ya Simba SC.

Kwa matokeo hayo, Singida KE sasa itamenyana na Yanga SC (Mwananchi) katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB 2025. Yanga SC ilitinga fainali baada ya kupata ushindi katika nusu fainali ya kwanza.
Kwa kuhitimishwa kwa Simba SC katika kinyang’anyiro hiki, Singida Black Stars inajiandaa kuvaana na Yanga SC katika fainali inayotarajiwa kuwa ya kipekee. Mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu fainali ya msimu wa 2025 CRDB Federation Cup.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako