Singida Black Stars Wafuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika Kwa Mara ya Kwanza

Singida Black Stars Wafuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika Kwa Mara ya Kwanza, Singida Black Stars Waandika Historia CAF Confederation Cup 2025/26.

Singida Black Stars Wafuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika Kwa Mara ya Kwanza

Timu ya Singida Black Stars imeweka historia kubwa katika soka la Tanzania baada ya kufanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup 2025/26). Hii inakuja baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Flambeau du Centre ya Burundi katika mchezo wa marudiano uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Matokeo ya Jumla (Aggregate): 4-2 kwa Faida ya Singida Black Stars

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Burundi, Singida Black Stars walionyesha ubora mkubwa kwenye mchezo wa nyumbani, wakitawala mchezo kwa asilimia kubwa na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa kishindo wa 3-1, na hivyo kufuzu kwa jumla ya 4-2.

Singida Black Stars Wafuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika Kwa Mara ya Kwanza
Singida Black Stars Wafuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika Kwa Mara ya Kwanza

Wafungaji wa Magoli

Muaku
Clatous Chama
Diomande

Kwa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26, Singida Black Stars imeandika sura mpya katika historia ya soka la Tanzania. Mafanikio haya yanathibitisha ukuaji wa klabu changa na kudhihirisha kuwa Tanzania sasa ni miongoni mwa mataifa yenye ushindani mkubwa katika mashindano ya vilabu barani Afrika.

CHECK ALSO:

  1. CV ya Pedro Gonçalves Kocha Mpya wa Yanga 2025
  2. Pedro Gonçalves Ndiyo Kocha Mpya wa Yanga SC
  3. Timu Zilizofuzu Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26
  4. Kikosi cha Simba vs Nsingizini Leo 26/10/2025