Stand United Yaibana Geita Gold, Yapenya Play Off ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025 | Timu ya Stand United inayofahamika kwa jina la Chama la Wana imefuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) baada ya kuifunga Geita Gold FC kwa jumla ya mabao 4-2. Ushindi huo umekamilika leo kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Katika mchezo wa mkondo wa pili, Stand United FC walipata mabao ya Yusuph Seleman ‘Mashaka’ kipindi cha kwanza na Omary Ramadhani la pili. Mchezo huo ulichezeshwa na waamuzi Ramadhani Kayoko, Frank Komba, na Glory Tesha.
Stand United Yaibana Geita Gold, Yapenya Play Off ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025

- Mchezo wa kwanza: Geita Gold 2 – 2 Stand United
- Mchezo wa marudiano: Stand United 2 – 0 Geita Gold
- Matokeo ya Jumla: Stand United FC 4 – 2 Geita Gold FC
Ushindi huu unaifanya Stand United kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazopigania nafasi ya kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026.
Play-off dhidi ya timu ya Premier League
Stand United FC sasa inasubiri timu itakayopoteza mchezo wa mchujo wa kushuka daraja Ligi Kuu ya NBC ili kuvaana nayo kwenye fainali. Mechi hiyo ya mikondo miwili imepangwa kufanyika Julai 3 na 7, 2025.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako