TAARIFA KWA WASIOITWA KWENYE USAILI TRA

TAARIFA KWA WASIOITWA KWENYE USAILI TRA
Dar es Salaam, 23 Machi, 2025: Kufuatia tangazo la kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika lililotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tarehe 22.03.2025, TRA inapenda kuwafahamisha waombaji ambao hawajaitwa kwenye usaili na mchujo, lakini wanadhani wana sifa za nafasi walizoziomba, kuwa wanapaswa kuwasilisha barua zao za malalamiko kwa Kamishna Mkuu wa TRA ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 24 hadi 25 Machi 2025.
Barua hizo zinapaswa kueleza sababu za waombaji kudhani kuwa wanastahili kuitwa kwenye usaili, pamoja na nyaraka kama nakala ya barua ya maombi ya kazi na vyeti husika.
Waombaji wanapaswa kutuma barua hizo kupitia barua pepe:
📧 huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz
Kwa waombaji waliopo Mkoa wa Dar es Salaam, barua zinaweza kupelekwa kwa mkono katika ofisi za TRA katika kitengo cha Huduma kwa Mlipa Kodi, kilichopo Mtaa wa Samora katika jengo la NHC HOUSE, jirani na makao makuu ya TTCL ndani ya saa za kazi.
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 Simu Bure: 0800 750 075 / 0800 780 078 / 0800110016
📱 WhatsApp: 0744 23 33 33
📧 Barua pepe: huduma@tra.go.tz / services@tra.go.tz
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa na:
IDARA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA
CHECK ALSO:
Weka maoni yako