Taifa Stars Yaelekea Morocco Mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia 2026 | Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeondoka kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wao wa Kundi E wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Taifa Stars Yaelekea Morocco Mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia 2026
Taifa Stars itamenyana na wenyeji wao, timu ya taifa ya Morocco, maarufu kwa jina la Atlas Lions, katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Machi 25, 2025, saa 6:30 mchana. Saa za Afrika Mashariki, sawa na macheo ya Machi 26, 2025.
Mechi hii ni muhimu kwa Taifa Stars katika harakati zake za kufuzu Kombe la Dunia 2026. Morocco, moja ya timu zenye rekodi bora barani Afrika, itakuwa mpinzani mgumu kwa Stars, lakini timu ya Tanzania ina matumaini ya kufanya vyema katika mechi hii ya ugenini.

Mashabiki wa soka wanatarajia mechi ngumu na yenye ushindani, ambapo Taifa Stars itatafuta matokeo mazuri dhidi ya wababe hao wa soka barani Afrika.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako