Taifa Stars Yapewa Pointi Tatu Dhidi ya Congo Brazzaville, Kufuzu Kombe la Dunia 2026: Taifa Stars yapata pointi tatu dhidi ya Congo Brazzaville katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeipa Tanzania ushindi wa pointi tatu, mabao matatu (3-0) dhidi ya timu ya Taifa ya Congo Brazzaville baada ya wapinzani wao kushindwa kushiriki mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 iliyopangwa kufanyika Machi.
Taifa Stars Yapewa Pointi Tatu Dhidi ya Congo Brazzaville, Kufuzu Kombe la Dunia 2026
Mechi hiyo ilipangwa Kundi E la timu ya Afrika ya kufuzu kwa raundi ya awali ya Kombe la Dunia 2026. Hata hivyo, haikuweza kuchezwa kutokana na Congo Brazzaville kufungiwa na FIFA kwa ukiukaji wa kiutawala na taratibu.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya FIFA, timu ambayo haitashiriki mechi bila sababu za msingi inapoteza 3-0, na pointi zote zinatolewa kwa timu pinzani. Tanzania kupitia Taifa Stars imenufaika na uamuzi huo kwa kujiongezea pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa makundi.
FIFA imethibitisha kuwa marufuku dhidi ya Congo Brazzaville imeondolewa, na kuruhusu timu hiyo kuendelea kushiriki katika awamu zijazo za mchujo.

Tanzania imenufaika na mapungufu ya kiutawala ya mpinzani wake, lakini bado inatakiwa kuendelea kujipanga vyema katika mechi zilizosalia. Njia ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 bado ni ndefu na inahitaji maandalizi makubwa na mshikamano wa kitaifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako