Taifa Stars Yapiga Kambi Afrika Kusini kwa Mechi ya Kirafiki na COSAFA 2025 | Taifa Stars imewasili Afrika Kusini kujiandaa na mechi ya Bafana Bafana na COSAFA 2025.
Taifa Stars Yapiga Kambi Afrika Kusini kwa Mechi ya Kirafiki na COSAFA 2025
Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kwa jina la Taifa Stars ipo nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Bafana Bafana na kushiriki michuano ya Kombe la Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) 2025.
Mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Afrika Kusini utapigwa Juni 6, 2025. Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya COSAFA, pamoja na mechi zijazo za kimataifa za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia.

Ratiba ya Mashindano ya COSAFA 2025 kwa Taifa Stars
Katika hatua ya makundi ya michuano ya COSAFA 2025, Taifa Stars imepangwa kucheza dhidi ya timu zifuatazo:
Tanzania vs Eswatini
Tanzania vs Madagascar
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na hushirikisha mataifa kutoka ukanda wa Kusini mwa Afrika. Ingawa Tanzania si mwanachama wa kudumu wa COSAFA, imealikwa kushiriki tena kama ilivyowahi kufanya katika miaka ya nyuma na kuchukua nafasi ya Morocco.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako