Taifa Stars Yatinga Hatua ya Robo Fainali CHAN 2024

Taifa Stars Yatinga Hatua ya Robo Fainali CHAN 2024: Baada ya Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Madagascar. Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeweka historia kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN 2024) baada ya kuifunga Madagascar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars Yatinga Hatua ya Robo Fainali CHAN 2024

Katika hatua ya makundi, Taifa Stars ilifunga mabao yote mawili ya mshambuliaji wake nyota, Clement Mzize, dakika ya 13 na 20, kabla ya Gregasse wa Madagascar kufunga bao la kufutia machozi dakika ya 33.

Ushindi huu umeifanya Tanzania kufikisha pointi tisa baada ya mechi tatu, huku ikiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika kundi lao. Hii imeiwezesha Taifa Stars kufuzu kwa robo fainali ya CHAN kwa mara ya kwanza katika historia yake, pia kuwa timu ya kwanza kufika hatua hiyo katika toleo la 2024.

Taifa Stars Yatinga Hatua ya Robo Fainali CHAN 2024
Taifa Stars Yatinga Hatua ya Robo Fainali CHAN 2024

Uwanja huo uliokuwa umejaa mashabiki ulishuhudia mechi ya hali ya juu, ambapo wachezaji wa Taifa Stars walionyesha nidhamu, mshikamano na nia kubwa ya kutaka kushinda. Mafanikio hayo yanaipa Tanzania matumaini mapya ya kufanya vizuri zaidi na kusonga mbele katika hatua zinazofuata za mashindano hayo muhimu ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.

CHECK ALSO:

  1. Makundi ya Droo ya Kombe la Shirikisho la CAF 2025/26
  2. RATIBA ya CAF Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
  3. Makundi ya Droo Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/26
  4. Orodha ya Vilabu Vitakavyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/26