TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025

TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025: TAMISEMI Yatangaza Orodha ya Walimu wa Kujitolea Waliochaguliwa 2025.

TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza majina ya walimu 128 waliopangiwa kujaza nafasi za walimu wa kujitolea katika shule za msingi baada ya nafasi hizo kubaki wazi kutokana na baadhi ya waombaji walioteuliwa awali kushindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi tarehe 14 Oktoba 2025 na Katibu Mkuu wa TAMISEMI, kutoka ofisini kwake iliyopo Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma.

TAMISEMI imeeleza kuwa nafasi hizi zilitolewa kwa walimu waliokuwa wameomba nafasi za kujitolea kuanzia tarehe 18 hadi 31 Agosti 2025, ambapo nafasi za awali zilijazwa. Hata hivyo, kutokana na baadhi ya walimu kushindwa kuripoti, nafasi hizo zimejazwa upya na waombaji wapya waliokidhi vigezo, ambao pia waliwasilisha maombi yao awali kati ya tarehe 17 – 30 Mei 2025.

TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025
TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025

Orodha kamili ya majina ya walimu 128 waliokidhi vigezo imewekwa kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI: 👉 www.tamisemi.go.tz

Walimu wote waliopata nafasi hizi wanatakiwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri katika maeneo waliyopangiwa kuanzia tarehe 15 hadi 21 Oktoba 2025.
Lengo la kuripoti ni kusaini Mkataba wa Ajira ya Kujitolea, kupokea barua za kupangiwa kituo cha kazi, na kuwasilisha vyeti halisi (Original Certificates) kwa uthibitisho/TAMISEMI Yatangaza Walimu 128 Waliochaguliwa Nafasi za Kujitolea 2025.

Kwa waombaji ambao majina yao hayajaorodheshwa katika tangazo hili, TAMISEMI imefafanua kuwa hawakupata nafasi katika awamu hii. Hivyo, wanashauriwa kufuatilia matangazo mengine yajayo kupitia tovuti ya TAMISEMI kwa fursa zaidi za ajira au kujitolea.

CHECK ALSO: