Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025 | Fursa Mpya za Watumishi wa Afya Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeendelea na jitihada za kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania kwa kuajiri wataalamu wapya katika sekta hiyo muhimu.
Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025
Katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, wito wa Kuajiri Watumishi wa Afya 2025 ulizinduliwa rasmi, ukiwalenga wataalamu kutoka sekta mbalimbali za afya wanaoomba kuajiriwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati kote nchini.
Lengo la ajira hizo ni kuongeza nguvu kazi ya kitaaluma ili kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa vijijini na maeneo ya pembezoni ambayo bado yanakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa afya.

Maelezo Muhimu Kuhusu Nafasi za Ajira za Afya 2025
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, nafasi hizi zitajumuisha kada mbalimbali zikiwemo:
Madaktari Bingwa na Madaktari wa kawaida
Wauguzi (Ngazi ya Shahada, Stashahada na Cheti)
Wafamasia
Wataalamu wa Maabara ya Afya
Wataalamu wa Mionzi
Wataalamu wa Lishe
Wataalamu wa Afya ya Jamii
Wateknolojia wa Dawa na Vifaa Tiba
Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHWs)
Ajira hizi ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya, bila kujali mahali alipo/Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025.
Vigezo na Masharti kwa Waombaji
Waombaji wa nafasi hizi wanapaswa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
Kuwa Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
Kuwa na vyeti halali vya taaluma kutoka chuo kinachotambulika na Baraza husika.
Kuwa na usajili wa kitaaluma kutoka bodi au baraza husika (mfano, Baraza la Madaktari, Baraza la Wauguzi n.k.)
Kuwa na cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Kuwa tayari kufanya kazi katika maeneo yoyote yatakayopangwa na Serikali, hasa katika vituo vya afya vilivyopo pembezoni.
Wizara ya Afya imetangaza kuwa maombi yote yatawasilishwa kupitia tovuti rasmi ya manunuzi ya serikali, ambapo waombaji wanapaswa kujisajili, kukamilisha taarifa zao na kupakia nakala za vyeti vinavyohitajika/Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025.
Tarehe rasmi ya ufunguzi wa maombi, pamoja na tarehe ya mwisho ya kutuma maombi, imeelezwa kwa kina katika tangazo kamili lililochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
CHECK ALSO:
Weka maoni yako