Tangazo la Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ 2025

Tangazo la Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ 2025 | Kidato cha Nne, Sita, Vyuo na Madaktari.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza rasmi nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa za kielimu kuanzia Kidato cha Nne hadi elimu ya juu, wakiwemo pia madaktari bingwa wa binadamu.

Tangazo hilo limetolewa leo, Aprili 30, 2025, katika Makao Makuu ya JWTZ yaliyopo Msalato, Jijini Dodoma. Kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob John Mkunda, taarifa hiyo ilisomwa na Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Gaudentius Ilonda.

Tangazo la Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ 2025

Vigezo vya Umri na Elimu kwa Waombaji:

  • Kidato cha Nne na Sita: Umri usizidi miaka 24

  • Stashahada (Diploma): Umri usizidi miaka 26

  • Shahada ya Elimu ya Juu: Umri usizidi miaka 27

  • Madaktari Bingwa wa Binadamu: Umri usizidi miaka 35

Tangazo la Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ 2025
Tangazo la Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ 2025

Utaratibu wa Kutuma Maombi:
Maombi yote lazima yaandikwe kwa mkono na yatumwe kuanzia tarehe 1 Mei 2025 hadi tarehe 14 Mei 2025. Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nyaraka muhimu kama ifuatavyo:

  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na namba

  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa

  • Vyeti vya kuhitimu masomo ya sekondari (Kidato cha Nne au Sita)

  • Vyeti vya masomo ya chuo (Stashahada/Shahada)

  • Namba ya simu ya mawasiliano iliyo hai

Jeshi la Wananchi wa Tanzania limeonya wananchi dhidi ya vitendo vya udanganyifu vinavyohusiana na ajira. Hakuna malipo yoyote yanayostahili kutolewa kwa mtu yeyote ili kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.

“Nitoe angalizo kwa wananchi: Hakuna nafasi ya kuandikishwa Jeshini kwa kutoa fedha. Msikubali kutapeliwa,” amesema Kanali Gaudentius Ilonda.

JWTZ imekuwa ikisisitiza kila mwaka kuwa mfumo wa ajira katika Jeshi ni wa haki, wazi na hauhusishi njia za mkato. Wananchi wanahimizwa kufuata utaratibu rasmi uliotolewa.

CHECK ALSO: