Tigo Pesa yabadilisha Jina, Yaitwa MIXX BY YAS

Tigo Pesa yabadilisha Jina, Yaitwa MIXX BY YAS | Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania ambayo leo imetangaza kubadili jina lake kutoka TIGO hadi kuitwa jina jipya la YAS (@yas_tanzania_), imetangaza mabadiliko ya jina kwenye bidhaa yake ya TIGO PESA ambayo kuanzia leo itakuwa ikiitwa MIXX BY YAS.

Mabadiliko haya yametangazwa na Uongozi wa Kampuni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo mchana ambayo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa.

Tigo Pesa yabadilisha Jina, Yaitwa MIXX BY YAS
Tigo Pesa yabadilisha Jina, Yaitwa MIXX BY YAS

Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina katika miaka yake yote thelathini ya huduma bora Nchini Tanzania ambapo awali ilikua ikiitwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS !

Taarifa zaidi kuhusu mabadiliko haya na vitu vyote ambavyo Wateja wa YAS wanatakiwa kufahamu nitaendelea kuviweka hapa katika kurasa za millardayo.

ANGALIA PIA: