Tuzo za Ballon dOr 2025 Kufanyika Septemba 22 Paris

Tuzo za Ballon d’Or 2025 Kufanyika Septemba 22 Paris, Orodha ya Tuzo na Wachezaji Wanaotajwa: Sherehe za Tuzo za Ballon d’Or 2025 zitafanyika Septemba 22, 2025, kwenye Ukumbi maarufu wa Théâtre du Châtelet jijini Paris, Ufaransa.

Tukio hili muhimu litawakutanisha nyota wa soka kutoka sehemu mbalimbali duniani kuwania tuzo mbalimbali zinazotolewa kwa wachezaji na makocha waliofanya makubwa katika soka mwaka huu.

Toleo hili la 69 tangu kuundwa kwa tuzo hizo linaendelea kudumisha sifa ya Ballon d’Or kama tuzo kongwe zaidi katika historia ya soka, inayosimamiwa na jarida maarufu la soka la France Football, ambalo lilizindua tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka wa 1956.

Tuzo za Ballon dOr 2025 Kufanyika Septemba 22 Paris

Tuzo Zitakazotolewa Ballon d’Or 2025

Katika hafla hiyo, tuzo mbalimbali zitakazotolewa ni kama ifuatavyo:

  • Ballon d’Or (Mchezaji Bora wa Dunia – Wanaume)

  • Ballon d’Or Féminin (Mchezaji Bora wa Dunia – Wanawake)

  • Kopa Trophy (Mchezaji Bora Chipukizi)

  • Yashin Trophy (Kipa Bora kwa Wanaume na Wanawake)

  • Gerd Müller Trophy (Mfungaji Bora – Klabu na Timu ya Taifa)

  • Johan Cruyff Trophy (Kocha Bora – Timu za Wanaume na Wanawake)

  • Club of the Year (Klabu Bora ya Mwaka – Wanaume na Wanawake)

  • Sócrates Award (Tuzo ya Mchezaji kwa Mchango wa Kijamii)

Majina ya wachezaji watakaowania tuzo hizo yanatarajiwa kutangazwa rasmi mapema mwezi Agosti 2025. Tayari mashabiki na wachambuzi wa soka wameanza kuwataja wachezaji wanaoweza kuwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo hizo. Miongoni mwa majina yanayozungumziwa sana ni pamoja na:

  • Kylian Mbappé

  • Lamine Yamal

  • Raphinha

  • Ousmane Dembélé

Wachezaji hawa wametajwa kutokana na kiwango bora walichoonyesha katika msimu huu, katika michuano ya ligi, mashindano ya kimataifa, na Kombe la Mataifa mbalimbali.

CHECK ALSO: