Twiga Stars Wabeba Kombe la CECAFA 2025 Baada ya Kuifunga Kenya 1-0 | Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania maarufu kwa jina la Twiga Stars wametawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya CECAFA kwa Wanawake 2025 baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Kenya katika mchezo wa fainali uliochezwa leo.
Bao pekee katika mechi hiyo lilifungwa na fowadi Clara Luvanga, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, katika dakika ya 48. Bao hili lilitosha kuipa Twiga Stars ushindi muhimu na kubeba kombe hilo la kihistoria.
Twiga Stars Wabeba Kombe la CECAFA 2025 Baada ya Kuifunga Kenya 1-0
Tanzania 1-0 Kenya
📅 Tarehe: 21 Juni 2025
⚽ 48’ – Clara Luvanga
Huu ni ushindi wa kihistoria unaodhihirisha ukuaji wa soka la wanawake nchini Tanzania na juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kuinua kiwango cha wachezaji wa kike.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako