Uandikishaji wa Kujiunga na Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ na JKT: Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) sasa linapokea maombi ya vijana wa Kitanzania wanaotaka kujiunga na jeshi mwaka 2025. Huu ni mwaliko rasmi kwa wale wote waliokidhi vigezo vya kuomba kwa kufuata utaratibu rasmi uliowekwa na TPF Makao Makuu.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limetangaza nafasi za kazi kwa vijana wa Kitanzania watakaochaguliwa kwenye usaili maalum mwaka 2025.
Uandikishaji wa Kujiunga na Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ na JKT
Maelekezo ya Jumla kwa Waombaji:
Maombi yawasilishwe kwa kuandika barua rasmi ya kuomba nafasi, ikieleza dhamira ya kujiunga na Jeshi.
Ambatanisha nakala za:
Cheti cha kuzaliwa
Vyeti vya elimu (kidato cha nne/kidato cha sita/vyuo)
Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
Picha ndogo (passport size)
Waombaji wote watajulishwa siku ya usaili baada ya uchambuzi wa awali.

Sifa za Kujiunga na JWTZ:
Mtu yeyote atakayehitaji kujiunga na JWTZ lazima atimize masharti yafuatayo:
Awe raia wa Tanzania.
Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na awe amefaulu.
Awe hajaoa wala hajaolewa.
Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 25.
Awe na tabia njema na mwenendo mzuri.
Awe na akili timamu na afya njema ya mwili na akili.
Nafasi za Maafisa (Officer Cadet):
Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board) huchagua askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea waliopo vikosini au waliotoka kwenye shule za askari wapya (Recruitment Schools).
Watakaochaguliwa hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet).
Maafisa hao hupelekwa katika Chuo cha Kijeshi cha Tanzania (Tanzania Military Academy – TMA) kwa mafunzo ya mwaka mmoja.
Anuani ya Kutuma Maombi Ya Uandikishaji wa Kujiunga na Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ na JKT:
Tanzania People’s Defense Force (TPDF)
P.O Box 194
Miyubi / Msalato
Dodoma – Tanzania
CHECK ALSO:
Weka maoni yako