Uhamiaji Yatangaza Nafasi za Ajira, Hivi Hapa Vigezo | Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, anatangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-
Uhamiaji Yatangaza Nafasi za Ajira, Hivi Hapa Vigezo
1. SIFA ZA MWOMBAJI
i.Awe ni raia wa Tanzania;
ii.Awe amehudhuria na kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au tayari amerudi Uraiani;
iii.Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
iv.Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
v.Awe na Kitambulisho cha Taifa au Nambari ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
vi.Awe na siha njema ya mwili na akili iliyothibishwa na Daktari wa Serikali,
vii.Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
viii.Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
ix.Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
x.Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
xi.Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 23, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 26 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
xii.Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
xiii.Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la ajira.
2. MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:
Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:-
Masijala, Udereva, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Tathmini na Uperembaji (Monitoring & Evaluation),Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa AC, Uhusiano, Cyber Security, Brass band, Mtunza Nyumba (House keeping), Mtunza Bustani (Garderner) na Mpiga chapa;
Weka maoni yako